Maombi Nachangamka

[1]
Saa heri ya maombi, sasa kwako tunarudi,
Sumbuku ya kuondoa, shida zitu na pungufu.
Taabuni mara nyingi, roho zetu zimepona,
Mashakani tumeshinda, wakati wa saa tamu.

[2]
Saa heri ya maombi, Twapelika dhiki zetu
Kwake aliyeahidi kubariki wenye haja.
Huagiza tumwendee, tutegemee neno lake,
Hivyo tumwekee yote, wakati wa saa tamu.

[3]
Saa heri ya maombi, tutazidi kuingia
Bomani mwetu na ngome, hata tuishapo mwendo.
Yesu atatusikea, tutamtafuta daima,
Na tutakapolutana tutamwona—saa tamu!