Mwendo Gani Nyumbani?

[1]
U mwendo gani nyumbani? Mlinzi akanijibu,
“Usiku sasa waisha,machweo karibu.”
Usihuzunike tena, bali ulemee mwendo
Hata ushike ufalme kule mwangani juu.

[2]
Na tena niliuliza, nchi yote ikajibu:
“Sasa mwendo watimika, milele karibu.”
Usihuzunike tena, ishara kuu zasonga
Na viumbe vyangojea sauti ya Bwana.

[3]
Nikamwuliza shujaa, ndivyo kanitia moyo:
“Shikilia mapigano, kitambo yaisha.”
Usihuzunike tena, kazi ifanye kwa moyo;
Tumeahidiwa tunu tuishapo shinda.

[4]
Siyo mbali na nyumbani! Fikara tamu njiani,
Latupoza roho, nalo lafuta machozi
Usihuzunike tena, kitambo tutakutana
Wenye furaha kamili nyumbani mwa Baba.