Mtakatifu

Language: Swahili
Nyimbo za Kristo

Mtakatifu

[1]
Roho Mtakatifu, Kiongozi amini;
Utushike mkono Tulio wasafiri;
Utupe kusikia Sauti ya upole:
“Msafiri fuata, Naongoza nyumbani.“

[2]
Wewe ndiwe rafiki, Msaada karibu;
Tusiache shakani; Na tukiwa gizani
Utupe kusikia Sauti ya upole:
“Msafiri fuata, Naongoza nyumbani.“

[3]
Siku zetu za ka zi, Zikiwa Zimekwisha,
Wala hatuna tamaa Ila mbingu na sala:
Utupe kusikia Sauti ya upole:
“Msafiri fuata, Naongoza nyumbani.“