uje kwetu

Language: Swahili
Nyimbo za Kristo

uje kwetu

[1]
Umetuahidi kwamba wawili Watatu, Kwa jina lako wakija,
Utawabariki; kwa hivi leo magoti nyumbani pako.

Yesu uje kwetu Utubariki;
Yesu uje kwetu Uwe karibu.

[2]
Umekuwa nasi siku nyingine Tunakuhitaji mpaka mwisho,
Uje Mkombozi; tupe neema; Tusikie Yesu, utubariki.

[3]
Uje utawale sauti zetu: Nyimbo, nazo sala uziagize.
Imani izidi, ikamilike; Pendo liwe safi, na njia nuru.