niangalie

Language: Swahili
Nyimbo za Kristo

niangalie

[1]
‘Uniangalie‘ atwambia Yesu aliyetufia;
Msalabani ni uzima, Hapa utaipata hazina.

Kutazama Kalwari, Kutazama Kalwari,
Ni kupewa kuishi Kuutazama mti.

[2]
Ninapojaribiwa ghafla, Shetani hatanitenga;
Nikitazama msalaba Nguzu nitaipata kwa Bwana.

[3]
Msalaba nitautazama Kila wakati, daima.
Ahadi nitategemea, Hovi kabisa sitaangukaa.