upendo

Language: Swahili
Nyimbo za Kristo

upendo

[1]
Vitu vyote ni sawa, panapo pendo;
Kila sauti tamu, panapo pendo.
Pana amani pale, na furaha nyumbani,
Siku zote salama. Panapo pendo.

Panapo upendo—
Siku zote salama,
Panapo pendo.

[2]
Furaha i nyumbani, panapo pendo;
Hapana machukizo, panapo pendo;
Chakula ni kitamu, mashamba ya sitawi,
Maisha ni kamili, panapo pendo.

[3]
Hata mbingini juu, pana furaha
Wakiona upendo nyumbani mwetu.
Macho yanapendezwa na viumbe vya Mungu,
Naye Mungu huona, panapo pendo.

[4]
Ee Yesu niwe wako, wako kabisa,
Ndipo patakuwako Pendo nyumbani;
Nitakaa salama, sitaifanya dhambi;
Nitabarikiwa tu panapo pendo.