Maneno Mabaya Yasitoke

[1]
Hasha, maneno mabaya yasitoke kinywani
Moyo mwema uzuie Ndimi, zisichafuke.

“Nanyi pendeni”, Asema Yesu,
(Mpendane) (Mpendane)
Kama mwanzo alivyotupenda:
“Nanyi pendeni”, alivyotupenda:
(Mpendane) (Mpendane)
Wana, tiini amri hii. (amri heri hii).

[2]
Pendo ni mtakatifu; Urafiki; mzuri:
Visiharibike mara kwa kunena vibaya.

[3]
Tusinene kwa hasira, inazaa huzuni,
Pendo lako ee mwokozi, Inatosha tushindi.