Nyota Tajini?

Language: Swahili
Nyimbo za Kristo

Nyota Tajini?

[1]
Leo ninafikiri ya nchi nzuri Ninayotaka kuiona;
Nisimamapo karibu na Mwokozi, Tajini zitakuwa nyota?

Sijui tajini mwangu kama nyota
Zitang‘aa kila wakati!
Nitakapoamka katika majumba,
Zitakuwa nyota tajini?

[2]
Kwa nguvu za Bwana nitafanya kazi, Nitavuta roho za watu,
Ili niwe na nyota katika taji, Bwana anapotupa tunu.

[3]
Nitakuwa na Furaha nikimwona, Kuweka miguuni pake
Watu waliovutwa kwa ajili ya Kazi yangu na Roho yake.