Ndani Yangu

Language: Swahili
Nyimbo za Kristo

Ndani Yangu

[1]
Tawala ndani yangu, Ee Yesu, Mfalme.
Uwe kwangu majibu kwa maswali yangu;
Uishi ndani yangu, Wewe, mwoongozi.
Utumishi ni wangu, Wako utukufu.

[2]
Hekalu nimetoa, Umelisafisha;
Sasa fahari yako Imulike ndani;
Dunia iwe kimya, mwili sasa uwe
Mtumwa mtulivu Wa kukutii tu.

[3]
Viungo vyake mwili, Vyote vikungoja
Tayari vikuutwa Kwenda, kusimama;
Bila manumguniko au malaumu,
Au kusumbuliwa, Pasipo majuto.

[4]
Niwe na utulivu pasipo haraka;
Tayari kungojea maagizo yako.
Tawala ndani yangu, Ee Yesu, Mfalme,
Uwe kwangu majibu kwa maswali yote.