Pa Mwokozi

Language: Swahili
Nyimbo za Kristo

Pa Mwokozi

[1]
Msalabani pa Mwokozi hapo niliomba upozi,
Moyo wangu ulitakaswa, Na asifiwe.

Na asifiwe, Na asifiwe.
Alinikomboa kwa damu, Na asifiwe.

[2]
Chini ya mti msumbufu Niliomba utakatifu,
Alinikomboa kwa damu, Na asifiwe.

[3]
Kwa ajabu ninaokoka, Yesu anakaa moyoni;
Mtini alinifilia, Na asifiwe.

[4]
Damu ya Yesu ya thamani Huniokoa makosani;
Huniendesha wokovuni, Na asifiwe.