Mtakatifu, Mtakatifu

[1]
U Mtakatifu! Mungu Mwenyezi!
Alfajiri sifa zako tutaimba;
U Mtakatifu, Bwana wa huruma,
Mungu wa vyote hata milele.

[2]
Umtakatifu! Na malaika
Wengi sana wanakuabudu wote;
Elfu na maelfu wanakusujudu
Wa zamani na hata milele.

[3]
U Mtakatifu! ingawa giza
Lakuficha fahari tusiioone,
U Mtakatifu! Wewe peke yako,
Kamili kwa uwezo na pendo.