Kuamini

Language: Swahili
Nyimbo za Kristo

Kuamini

[1]
Ninao wimbo mzuri, Tangu kuamini;
Wa Mkombozi, Mfalme, Tangu kuamini.

Tangu kuamini, Jina lake ‘tasifu,
Tangu kuamini, Nita lisifu jina lake.

[2]
Kristo anitosha kweli, Tangu kuamini,
Mapenzi yake napenda, Tangu kuamini.

[3]
Ninalo shuhuda sawa, Tangu kuamini;
Linalofukuza Shaka, Tangu kuamini.

[4]
Ninalo kao tayari, Tangu kuamini;
Nililorithi kwa Yesu, Tangu kuamini.