Kisa Cha Yesu

Language: Swahili
Nyimbo za Kristo

Kisa Cha Yesu

[1]
Nipe habari za Yesu, Kwangu ni tamu sana;
Kisa chake cha thamani Hunipendeza sana.
Jinsi malaika wengi walivyoimba sifa,
Alipoleta amani Kwa watu wa dunia.

Nipe habari za Yesu, Kaza moyoni mwangu;
Kisa chake cha thamani Hunipendeza sana.

[2]
Kisa cha alivyofunga Peke yake jangwani.
Jinsi alivyolishinda Jaribu la Shetani;
Kazi aliyoifanya, Na siku za huzuni,
Jinsi walivyomtesa: Yote ni ya ajabu!

[3]
Habari za Msalaba Aliposulubishwa;
Jinsi walivyo mzika Akashinda kaburi.
Kisa chake cha rehema. Upendo wake kwangu,
Aliyetoa maisha Nipokee wokovu.