inakuhitaji

Language: Swahili
Nyimbo za Kristo

inakuhitaji

[1]
Bwana ninakuhitaji! Nimpofu, maskini;
unishike mkononi, kwako napata nguvu

Kila saa, kila saa bwana ninakuhitaji;
Kila saa, kila saa unilinde kila saa.

[2]
Univike na mavazi ya usikivu wako;
Nguo zangu mi machafu, Nazitamani zako.

[3]
Wewe ukiniongoza nitakwenda salama;
Nenda nami siku zote, U nuru na uzima.

[4]
Na ikiwa m-beleni sehemu yangu ngumu,
Au ikiwa furaha, unilinde kila saa.