Msalaba

Language: Swahili
Nyimbo za Kristo

Msalaba

[1]
Naendea msalaba, Ni mnyonge, mpofu,
Yapitayo naacha nipe msalaba tu.

Nakutumaini tu, wee Mwana wa Mungu;
Nainamia kwako; Niponye sasa, Bwana.

[2]
Nakulilia sana: Nalemewa na dhambi;
Pole Yesu asema: “Nitazifuta zote.”

[3]
Natoa vyote kwako, nafasi nazo nguvu,
Roho yangu na mwili viwe vyako milele.

[4]
Kwa damu yake sasa amenivuta sana,
Upendo hubidisha, nimtafute Mwokozi.