Zaka Kwa Hazina

Language: Swahili
Nyimbo za Kristo

Zaka Kwa Hazina

[1]
Sikieni neno la Mungu Wetu, Zileteni zaka kwa hazina
Leteni na mioyo yenu yote; mibaraka itakuja.

Zileteni zaka kwa hazina, kanijaribu sasa nazo;
Nitakupeni mibaraka, zaidi ya nafsi ya kupewa.

[2]
Wataka Roho Mtakatifu kwako? Uzilete zaka kwa hazina
Ukae karibu na Bwana wako, ndipo utakapo barikiwa.

[3]
Je! Unakasoro na Bwana wako? Uzilete zaka kwa hazina
Uzilete kama alivyosema, Ndipo utakapo barikiwa.

[4]
Ushukuru Bwana na moyo wote, unapoleta zaka ghalani;
Usadiki ahadi zake zote, ndipo utakapo barikiwa.

[5]
Tuimbe sote nyimbo za furaha, tunapoleta zaka ghalani
Twimbe kabisa na furaha kubwa, kwani tutabarikiwa.