Zaidi

Language: Swahili
Nyimbo za Kristo

Zaidi

[1]
Ninakupenda zaidi, Ya vyote vingine;
Kwani umenipa raha, Na amani Bwana.

Nusu haijatangazwa (tangazwa)
Ya Upendo wako;
Nusu haijatangazwa (tangazwa)
Damu hutakasa (takasa)

[2]
Nakujua u karibu Kuliko dunia;
Kukukumbuka ni tamu Kupita kuimba.

[3]
Kweli wanifurahisha, Na nitafurahi;
Pasipo upendo wako Naona huzuni.

[4]
Itakuwaje Mwokozi, Kukaa na wewe,
Ikiwa ulimwenguni Tuna furaha hii?