yetu aliye mbinguni

[1]
Baba yetu aliye mbinguni,
Amenifurahisha yakini;
Kuniambia mwake Chuoni,
Ya kuwa nami Yesu pendoni.

Anipenda Mwokozi Yesu,
Anipenda, Anipenda:
Anipenda, Mwokozi Yesu,Anipenda mimi.

[2]
Nimuachapo kutanga mbali,
Yeye yu vivyo, hupenda kweli:
Hunirejeza kwake moyoni,
Kweli yu nami Yesu pendoni.

[3]
Anipenda! Nami ninampenda,
Kwa wokovu alionitenda;
Akanifilia Msalabani,
Kwa kuwa nami Yesu pendoni.