Yangu Amka Sasa

Language: Swahili
Nyimbo za Kristo

Yangu Amka Sasa

[1]
Roho yangu amka sasa, mara jitahidi;
Shindano ni lake Bwana, Zawadi ni taji.

[2]
Sauti ni yake Mungu inayokuita;
Ndiyo alitekirimu taji ya uzima.

[3]
Mashahidi ndio wengi wanaokuoma;
Ya nyuma usifikiri bali mwendo kaza.

[4]
Bwana umetuanzisha katika shindano;
Kwa vile tunaposhinda ushindi ni wako.