Ya Mwana

Language: Swahili
Nyimbo za Kristo

Ya Mwana

[1]
Tarumbeta ya mwana itakapolia mara,
Milele itakapopambazuka,
Nao wa haki watakapokusanyika ng‘ambo,
Majina yaitwapo, lo!—niweko.

Majina yaitwapo, lo!—
Majina yaitwapo, lo!—
Majina yaitwapo, lo!—
Majina yaitwapo, lo!—niweko.

[2]
Siku ile watakatifu watakapoamka
Na kuondoka huru kaburini
Watakapokusanyika makaoni kule juu,
Majina yaitwapo, lo—niweko.

[3]
Tutende kazi kwa yesu mchana kutwa kwa bidii,
Tutangaze kote pendo lake kuu,
Nayo kazi itakapotimika hap chini
Majina yaitwapo, lo—niweko.