Ya Msalaba

Language: Swahili
Nyimbo za Kristo

Ya Msalaba

[1]
Chini ya msalaba Nataka simama;
Ndio mwamba safarini, Wa kivuli chema;
Ni kweli kwa roho yangu Ni tuo kamili,
Tatua mzigo wangu Wakati wa hari.

[2]
Hapa ni pema sana, Ni ngome kamili;
Hapa yameonekana, Mapenzi ya kweli;
Kama alivyoonyeshwa Yakobo zamani,
Msalaba umekuwa ngazi ya mbinguni.

[3]
Na Yesu Msalabani Walimkemea,
Alikufa niokoke Niliyepotea:
Naona ajabu sana Ya mambo mawili
Jinsi alivyonipenda Nisiyestahili.

[4]
Atakayeonana Na Yesu mbinguni,
Njia yake aanzapo Ni Msalabani;
Wokovu upo hapa tu, Mwingine hapana,
Kisha kuna furaha kuu Pamoja na Bwana.