Wetu Yeye Mwamba

[1]
Mungu wetu yeye mwamba, Kimbilio taabuni;
Msaada penye shida ulio karibu sana.

Mwamba wetu kutupumzisha, yu kivuli kuburudisha
Yu Mwongozi katika njia, kimbilio taabuni.

[2]
Mchana usiku, yule kimbilio taabuni,
Hivyo hatutaogopa, kwani yu karibu sana.

[3]
Iwayo yote, Yeye tu kimbilio taabuni,
Twamjua Yeye Mlinzi aliye karibu sana.

[4]
Mungu wetu Ficho kwetu, kimbilio taabuni.
Siku zote uwe Boma lililo karibu sana.