wenye Imara

Language: Swahili
Nyimbo za Kristo

wenye Imara

[1]
Mwamba wenye imara Kwako nitajificha!
Maji hayo na damu Yaliyotoka humu,
Hunisafi na dhambi, Hunifanya mshindi.

[2]
Kwa kazi zote pia Sitimizi sheria.
Nijapo fanya bidii, Nikilia na kudhii,
Hayaishi makosa; Ndiwe wa kuokoa.

[3]
Sina cha mkononi, Naja msalabani;
Nili tupu, nivike; Ni mnyonge,nishike;
Nili mchafu naja, Nioshe ni sijafa.

[4]
Nikungojapo chini, Na kwenda kaburini;
Nipaapo mbinguni, Na kukwona enzini,
Roho yangu na iwe Rahani mwako wewe.