Wenye Dhambi

Language: Swahili
Nyimbo za Kristo

Wenye Dhambi

[1]
Katika wenye dhambi Ndimi mkuu wao—
Ila yesu akaja, Kwa dhanbi alikufa,
Akamimina damu Niupate uzima.

[2]
Ajabu pendo lake! Pendo lililo kuu,
Pendo lisilo mwisho, Lidumulo milele—
Lililonitafuta Inawa sikupenda.

[3]
Ingawa ni mbaya Kristo ni vyote kwangu;
Ajua haja zangu; Huzuni zangu, zake;
Hata katika vita, Akiwapo salama.