Watu

Language: Swahili
Nyimbo za Kristo

Watu

[1]
Walio kifoni, nenda waponye.
Uwatoe walio shimoni;
Wanaoanguka uwainue;
Habari njema uwajulishe.

Walio kifoni waokoeni,
Mwokozi yuko huwangojea

[2]
Wajapokawia anangojea,
Awasubiri waje tobani;
Mwokozi hawezi kuwadharau,
Huwasamehe tangu zamani:

[3]
Na ndani ya moyo wa wanadamu
Huwamo shida, tena huzuni;
Lakini kwa Yesu kuna rehema
Kuwaponya na kuwakoa.

[4]
Walio kifoni, nenda waponye
Kazi ni yetu, zawadi iko;
Nguvu kuhubiri Bwana hutoa
Kwa subira tuwavute sasa.