Wangu Uzima

Language: Swahili
Nyimbo za Kristo

Wangu Uzima

[1]
Twae wangu uzima sadaka ya daima;
Twae saa na usiku Zikutukuze huku.

[2]
Twae mikono nayo, ifanye upendayo,
Twae yangu miguu, Kwa wongozi wako tu.

[3]
Twae sauti yangu, niimbe kwa Mungu tu;
Itwae na midomo, Ijae neno lako.

[4]
Twae dhahabu pia Na yote ya dunia;
Twae yangu hekima, upendavyo tumia.

[5]
Nia itwae, Mungu, haitakuwa yangu;
Twae moyo; ni wako, uwe makazi yako.

[6]
Twae mapenzi yangu, sifa za moyo wangu;
Twae kabisa nafsi Niwe wako halisi.