wa kanisa

Language: Swahili
Nyimbo za Kristo

wa kanisa

[1]
Msingi wa Kanisa Ndiye Yesu Bwana;
Kiumbe chake kipya Akipenda sana;
Kutaka‘ kitafuta Alishuka chini,
Naye kwa haja yake, Akafa Mtini.

[2]
Lina kila kabila Kisha Ndiyo moja
Wokovu wake una Mwokozi mmoja;
Uzazi ni umoja, Moja tumaini.
Chakula ni kimoja, Moja tumaini.

[3]
Watu hustaajabu Kwa mashaka yote
Yaipatayo nje Hata ndani mwote;
Ila watakatifu Humwomba, wakikesha
Usiku ni kilio, Asubuhi raha.

[4]
Mashaka na taabu Hata vita vyake,
Vyangoja matimizo Ya amani Yake,
Ndipo kwa macho yetu Twone utukufu
Kanisa ya kushinda Itastarehe juu.