Upesi

Language: Swahili
Nyimbo za Kristo

Upesi

[1]
Anakuja upesi, Yesu Bwana wetu, Msafiri mbali na kwao;
Alisema dhahiri, “Nitakuja tena”; Amina; na uje, E Bwana.

Yuaja, Yesu atarudi sasa; Anakuja duniani.
Wasafiri wote watapumzika Yesu anaporudi tena.

[2]
Makaburi yote wafu wanapolala Yatafunguliwa tena;
Na mamilioni pale wataondoka tena, Wasione machozi kamwe.

[3]
Hatutatengana na hao tena huko; Nyimbo nzuri tutaimba.
Watakusanyika ‘toka kila kabila, Miguuni pa Mwana-kondoo.

[4]
Aleluya Amin! Aleluya tena! Upendo wake unashinda!
Tutamsifu milele, hata tutashangaa, Jinsi alivyo tukomboa.