Uniongoze Juu

Language: Swahili
Nyimbo za Kristo

Uniongoze Juu

[1]
Nakaza mwendo mbinguni, kila siku napanda juu;
Naomba nikisafiri, “Bwana uniongoze juu.

Bwana uniinue juu Kwa imani hata mbingu,
Juu kuliko dunia; Bwana uniongoze juu.

[2]
Moyo wangu hutaki Kukaa palipo shaka;
Wengine wapenda chini nia yangu ni ku panda.

[3]
Nataka kupanda juu Nisishindwe na adui;
Kwa imani nasikia sauti ya washindaji.

[4]
Kupanda juu nataka niuone utukufu;
Hata mwisho nitaomba, “Bwana uniongoze juu.”