Umo Mwoyoni.

Language: Swahili
Nyimbo za Kristo

Umo Mwoyoni.

[1]
Mlimani pana mwanga, Mwanga wa jua zuri
Shambani na bahari Jua tukufu liko;
Mwanga ulio mkubwa Umo moyoni mwangu,
Kwa kuwa Yesu alipo hapa pana mwangaza.

Mwangaza ulio mzuri, Mwanga umo moyoni;
Akiwapo Bwana Yesu pana mwanga moyoni.

[2]
Kama mavazi kikuu Ninavua Huzuni:
Nguo nzuri za furaha Umenipa za kuvaa.
Nakuandama rohomi Hata nyumba ya juu
Iliyopambwa vizuri Katika pendo lako.

[3]
Ulinikomboa Yesu; Maisha yangu, mali,
Vyote ni vyako, Mwokozi-Daima nikusifu.
Nakuandama rohomi Hata nyumba ya juu
Iliyopambwa vizuri Katika pendo lako.