Umechoka Sana?

Language: Swahili
Nyimbo za Kristo

Umechoka Sana?

[1]
Wewe umechoka sana? Wataka raha?
Kwake Yesu utapata –Msaada.

[2]
Alama anazo Yeye? Sana! Makovu
Ya mikono, na miguu, Na mbavu.

[3]
Naye amevikwa taji Kichwani mwake?
Taji, kweli, alivikwa –Miiba!

[4]
Huku nikimfuata, Nipate nini?
Maonjo nje, na ndani—Amani.

[5]
Kwamba namwandama Yeye, Mwisho ni nini?
Kurithi futaha naye---Milele.