ukimngojea

Language: Swahili
Nyimbo za Kristo

ukimngojea

[1]
Sijui atakapokuja,
Mchana au usiku;
Labda sa-a ya alasiri,
Pengine ni alfajiri.
Hutwambia tuwe tayari,
Ta-a zetu tusizime;
Ili ajapo atukute;
Tuwe tukimngoja Yeye.

[Tu - - - kimngojea - - - a,
(kukesha, tunakungoja Wewe)
Tu - - - kimngojea - - - a,
(kukesha, tunakungoja Wewe)
Tu - - - kimngojea - - - a,
(kukesha, tunakungoja Wewe)
Twakesha, twamngoja Yeye.

[2]
Nakumbuka huruma zake,
Bei ya wokovu wetu:
Aliacha nyumba tukufu
Awafilie wabaya.
Ninadhani itampendeza,
Kama sisi watu wake,
Tukionyesha pendo letu,
Tuwe tukimngoja Yeye

[3]
Ee Yesu, Mwokozi mpendwa,
Wajua nalihifadhi
Tumaini la kukuona.
La kukaribishwa nawe
Ukija kwa watu wengine,
Kama mhukumu wao,
Kwangu utakuwa rafiki,--
Nakesha, nakungojea.