Ufalme

Language: Swahili
Nyimbo za Kristo

Ufalme

[1]
Mrithi ufalme kwani walala?
Karibu wokovu wasinzia?
Amka simama uvae silaha
Haraka sana saa zapita.

[2]
Mrithi ufalme mbona ‘kawia‘?
M-bona hupokei zawadi?
Haya uvae, Mwokozi yuaja;
Haraka, umlaki apitapo.

[3]
Mataifa makuu ya dunia
Yapigana na kujiangusha.
Usiziofu dalili, Mrithi;
Ishara zotte hazikawii.

[4]
‘Sitazame anasa za dunia!
Kwani hayo ya pita upesi.
Zivunje kamba zinazokufunga.
Mrithi ufalme, njoo‘karudi.

[5]
Inua kichwa, tazama mbele tu.
M-falme aja na utukufu;
Jua la onekana milimani,
Warithi ufalme furahini.