Twakujia

Language: Swahili
Nyimbo za Kristo

Twakujia

[1]
Baba twakujia, Uwe msaada;
Uwe kimbilio, twakusihi.
Dunia ni giza tukitengwa nawe;
Tufariji hapa, Baba yetu.

Baba twakujia, tu dhahifu, usitugeue, tusikie.

[2]
Salama tulinde, kati ya taabu;
Uwe raha yetu mashakani.
Roho yasumbuka, Baba tujalie;
Twakuomba sana, tupe nguvu.

[3]
Neema utupe, tukubali kwako;
Moyo wetu linda, safarini;
Tuongoe mbele, tupate kushinda
Na Kufika ng‘ambo, kule kwako.