Tuonane Mtoni?

Language: Swahili
Nyimbo za Kristo

Tuonane Mtoni?

[1]
Ati twonane mtoni? maji mazuri ya mbingu;
Yanatokea mwangani, penye kiti cha Mungu.

Naam, twonane mtoni! Watakatifu, kwenu ni mtoni!
Tutakutanika kule mtoni penye kiti cha Mungu.

[2]
Tukitembea mtoni na Yesu mchunga wetu,
Daima tu ibadani usoni pake kwetu.

[3]
Tukisafiri mtoni tutue ulemeao,
Wema wa Mungu yakini: una taji na vao!

[4]
Kwang‘ara sana mtoni cha Mwokozi ni kioo,
Milele hatuachani tumsifu kwa nyimbo.

[5]
Karibu sana mtoni, karibu tuatawasili,
Mara huwa furahani na amani ya kweli.