Tumwabudu Mfalme Mtukufu

[1]
Na tumwabudu huyo mfalme,
sifa za nguvu zake ziimbe;
Ni ngao, ni ngome, Yeye milele,
Ndizo sifa zake kale na kale.

[2]
Tazameni ulimwengu huu,
Ulivyoumbwa, ajabu kuu;
Sasa umewekwa pahali pake,
Hata utimize majira yake.

[3]
Kwa ulinzi wako, kwetu Bwana,
Twakushukuru, U mwema sana;
Hupewa chakula kila kiumbe,
Kila kitu kina mahali pake.

[4]
Wanadamu tu wanyonge sana,
Twakutumaini Wewe, Bwana;
Kwamwe haupungui wako wema,
Mkombozi wetu, Rafiki mwema.