Tubariki

Language: Swahili
Nyimbo za Kristo

Tubariki

[1]
Tutokapo tubariki, Utupe Kufurahi;
Tuwe na Upendo wako, Neema ya kushinda.
Nawe utuburudishe Tukisafiri chini.

[2]
Twatoa sifa, Shukurani kwa neno ya injili;
Matunda ya wokovu Yaonekane kwetu;
Daima tuwe amini Kwa kweli yako, Bwana.

[3]
Siku zetu zikizidi Tuzitoe kwa Yesu;
Tuwe na nguvu moyoni Tusichoke njiani;
Hata tutakapoona Utukufu wa Bwana.