Sita Zimepita

Language: Swahili
Nyimbo za Kristo

Sita Zimepita

[1]
Siku sita zime pita, Sabato tena karudi;
Shangilie roho yangu, itukuze kwa busara.

[2]
Msifuni awapaye pumziko tamu wachovu,
Kwake roho yatulizwa, kupita siku nyingine.

[3]
Moyo wetu ufurahi, na kutoa mashukuru;
Ujalizwe raha ile, yasipitikwa kamwe.

[4]
Raha hiyo ya rohoni, ni amana ya pumziko
Ambalo limewekwa juu, kikomo cha masumbuko.