Sana

Language: Swahili
Nyimbo za Kristo

Sana

[1]
Karibu sana univute, karibu sana daima niwe.
Bwana napenda unishike, Unilinde nisitengwe nawe,
Unilinde nisitengwe nawe.

[2]
Karibu sana, sina kitu, Sina sadaka kwa Bwana Yesu,
Isipokuwa moyo wangu: Uutakase katika damu,
Uutakase katika damu.

[3]
Karibu sana, Wewe nami. Nima furahi kuacha dhambi----
Anasa zote na kiburi: Nipe Yesu niliyemsulibi,
Nipe Yesu niliyemsulibi.

[4]
Karibu sana. Hata mwisho. Hata mbinguni nisimamapo:
Daima dawamu niwepo Nitakapoona uso wako,
Nitakapoona uso wako.