Roho wa mbinguni

[1]
Ewe Roho wa Mbinguni, Maombi sikia
Makao yako yafanye mioyoni mwetu.

[2]
Kama nuru, tupenyeze, Giza uondoe;
Siri yako tuione, Na amani yako.

[3]
Kama moto, tusafishe, Choma dhambi yetu;
Roho zetu ziwe zote hekalu la Bwana.

[4]
Kama umande, na uje, Utuburudishe,
Moyo ‘kavu utakuwa Ni wenye baraka.

[5]
Kama upepo Ee Roho, Katika Pentekoste
Ukombozi utangaze, Kwa kila taifa.