Rafiki

Language: Swahili
Nyimbo za Kristo

Rafiki

[1]
Ninaye rafiki naye Alinipenda mbele;
Kwa kamba za pendo lake Nimefungwa milele;
Aukaza moyo wangu, Uache ugeuzi,
Ninakaa ndani yake, Yeye kiwangu, milele.

[2]
Ninaye Rafiki ndiye Aliyenifilia;
Alimwaga damu yake Kwa watu wote pia;
Sina kitu mimi tena, Nikiwa navyo tele;
Pia vyote ni amana Ndimi wake milele.

[3]
Ninaye Rafiki naye Uwezo amepewa;
Atanilinda mwenyewe, Juu ‘tachukuliwa;
Nikizama mbinguni Hupata nguvu tele;
Sasa natumika chini, Kisha juu milele.

[4]
Ninaye Rafiki naye Yuna na moyo mwema,
Ni Mwalimu, Kiongozi, Mlinzi wa daima;
Ni nani wa kunitenga Na mpenzi wa mbele?
Kwake nimetia nanga, Ndimi wake milele.