Pendo Lako

Language: Swahili
Nyimbo za Kristo

Pendo Lako

[1]
Niimbe (niimbe) pendo lake,
Pendo la (Pendo la) Yesu Bwana;
Sababu (Sababu) alitoka
Kwa Baba, akafa.

Niimbe (niimbe) pendo lake;
Sifa kuu (Sifa kuu) nitatoa;
Akafa (akafa) niwe hai,-----
Niimbe pendo lake.

[2]
Machozi (Machozi) alitoa
Ijapo (ijapo) sijalia;
Maombi (maombi) yangu bado,
Aniombeapo.

[3]
Upendo (upendo) kubwa huo!
Dunia (dunia) haijui
Samaha (samaha) kwa makosa
Kubwa kama yangu.

[4]
Hapana (hapana) tendo jema
Ambalo (ambalo) nilitenda,
Nataka (nataka) toka leo
Nimwonyeshe pendo.