Pake Yesu

Language: Swahili
Nyimbo za Kristo

Pake Yesu

[1]
Miguuni pake Yesu, Maneno yake tamu;
Pahali palipo heri, Niwepo kila siku.
Miguuni pake Yesu Nakumbuka upendo
Na hisani vyake kwangu, Vimenivuta moyo.

[2]
Miguuni pake Yesu, Hapa pahali bora
Pa kuweka dhambi zangu: Pahali pa pumziko.
Miguuni pake Yesu, Hapa nafanya sala,
Kwake napewa uwezo, Faraja na neema.

[3]
Unibariki Mwokozi, Ni miguni pako,
Unitazame kwa upendo Nione uso wako.
Nipe Bwana nia yake Ili ionekane
Nimekaa na Mwokozi Aliye haki yangu.