Pa Moyo

Language: Swahili
Nyimbo za Kristo

Pa Moyo

[1]
Mlangoni pa moyo; Mgeni! (Amesimama)
Amesimama pale, Mgeni! (Amesimama)
Umkaribishe sasa,
Umkaribishe Mwana
Wa Baba wa upendo: Mgeni! (Umkaribishe)

[2]
Moyo wako kwa Bwana, Fungua. (Fungulieni)
Asikuache mbali,Fungua. (Fungulieni)
Umkubali Rafiki,
Roho atafariji
Naye atakutunza:Fungua. (Fungukieni)

[3]
Usikie sauti Ya Bwana. (Uisikie)
Uyachague mambo Ya Bwana. (Mambo ya Bwana)
Ufungue mlango,
Usimwambie bado:
Jina lake tumai---- Yu Bwana. (Jina la Bwana)

[4]
Na ufungue moyo, Kwa Bwana (Fungulieni)
Utapewa msaada, Wa Bwana (Msaada wetu)
Uzuri utavikwa
Dhambi ataondoa,
Ukifungua moyo. Kwa Bwana (Fungulieni)