Ni Mapenzi

Language: Swahili
Nyimbo za Kristo

Ni Mapenzi

[1]
Mapya ni mapenzi hayo, Asubuhi tuonayo;
Saa za giza hulindwa, Kwa uzima kuamka.

[2]
Kila siku, mapya pia, Rehema, wema na afya,
Wokovu na msamaha, Mawazo mema, furaha.

[3]
Tukijitahidi leo Na mwendo utupasao,
Mungu atatueleza Yatakayompendeza.

[4]
Mamboyetu ya dunia Bwana atayang‘aria,
Matata atageuza Yawe kwetu ya baraka.

[5]
Yaliyo madogo, haya Bwana tukimfanyia,
Yatosha: tutafaidi Huvuta kwake zaidi.

[6]
Ewe Bwana, siku zote, Tusaidie kwa yote:
Mwendo wetu wote vivyo, Uwe kama tuombavyo.