naye Yesu

Language: Swahili
Nyimbo za Kristo

naye Yesu

[1]
Kufariki naye Yesu! Usingizi wenye heri;
Raha isifujika kwa majonzi na adui.

[2]
Kufariki naye Yesu! Lo! ya kubwaga simanzi
Na kulala na amani hata Bwana awatuze.

[3]
Kufariki naye Yesu! heri watakaoamshwa,
Wataona siku ile utukufu wake Bwana.

[4]
Kufariki naye Yesu! awaamka aitapo;
Watapasua kaburi na kutoka watukufu.