Nakupenda

Language: Swahili
Nyimbo za Kristo

Nakupenda

[1]
Yesu nakupenda, u mali yangu,
Anasa za dhambi sitaki kwangu;
Na Mwokozi aliye niokoa
Sasa nakupenda, kuzidi pia.

[2]
Moyo umejaa mapenzi tele
Kwa vile ulivyonipenda mbele,
Uhai wako ukanitolea
Sasa nakupenda, kuzidi pia.

[3]
Ulipo angikwa Msalabani
Tusamehewe tulio dhambini;
Taji ya miiba uliyoivaa,
Sasa nakupenda, kuzidi pia.

[4]
Mawanda mazuri na masikani
Niyatazamapo huko mbinguni,
Tasema na taji Nitakayovaa
Sasa nakupenda, kuzidi pia.