Na Yesu

Language: Swahili
Nyimbo za Kristo

Na Yesu

[1]
Yesu Mwokozi, kwa hakika . Hunipa furaha na amani;
Mrithi wa wokovu wake, Natakaswa kwa damu yake.

Habari hiyo wimbo wangu, Daima nitamsifu Yesu.
Habari hiyo wimbo wangu, Daima nitamsifu Yesu.

[2]
Nijitoapo nina raha, Na kwa imani namwona Bwana;
Aniletea malaika, Wananilinda niokoke.

[3]
Hali na mali anaitwaa, Katika Yesu nabarikiwa;
Nikimngoja kwa subira, Wema wake unanitosha.