Na Wewe, Mungu Wangu

[1]
Karibu na wewe, Mungu wangu:
Karibu zaidi Bwana wangu,
Siku zote niwe karibu na Wewe,
Karibu zaidi, Mungu wangu.

[2]
Mimi nasafiri duniani,
Pa kupumzika sipaoni,
Nilalapo niwe karibu na Wewe,
Karibu zaidi, Mungu wangu.

[3]
Yote unipayo yanivuta;
Pa kukaribia nitapata;
Na nielekezwe, karibu na Wewe,
Karibu zaidi, Mungu wangu.

[4]
Na kwa nguvu zangu nikusifu;
Mwamba, uwe maji ya wokovu
Mashakani niwe kaaribu na Wewe;
Karibu zaidi, Mungu wangu.

[5]
Na nyumbani mwa juu, Baba yangu
Nikinyakuliwa toka huko,
Kwa furaha niwe pamoja na Wewe,
Karibu zaidi, Mungu wangu.