Mwokozi, Twalitukuza Jina Lako

[1]
Tena, Mwokozi, twalitukuza
Jina lako lenye kupendeza,
Twakungojea neno la amani,
Kabla hatujakwenda nyumbani.

[2]
Tupe amani njiani mwetu.
Wewe u mwanzo, u mwisho wetu;
Dhambini kamwe isiingie
Midomo ikutajayo wewe.

[3]
Utupe amani usiku huu,
Ili gizani kuwe nuru kuu.
Tulinde kwa kuwa kwako Bwana.
Usiku ni sawa na mchana .

[4]
Tupe amani ulimwenguni
Ndiyo dawa yetu majonzini;
Na ikitwita sauti yako,
Tupe amani milele kwako.